Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii
Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kukabidhi uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa Rais wa Uganda Yoweri Museveni baada ya kumaliza muda wake.
Tanzania imemaliza uenyekiti wake baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga kukabidhi uenyekiti wa Mawaziri wa Afrika Mashariki kwa Uganda mwezi Aprili mwaka huu.
Dkt Mahiga amesema, Tanzania imekuwa Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo kwa miaka miwili mfululizo kwani baada ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumaliza muda wake, Wakuu wanchi wanachama wa jumuiya hiyo walimchagua Rais Magufuli kuendelea kuwa Mwenyekiti.
“Kwa hiyo pamoja na hilo lakini pia kuna mambo mengi ambayo tumejadiliana na mengine yatatolewa uamuzi na Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,” amesema Dkt. Mahiga.
Amesema karibu marais wa nchi zote wanachama wanatarajiwa watakuwepo isipokuwa Sudani Kusini ambayo imetoa udhuru.
Marais ambao wamethibitisha kuhudhuria ni pamoja na Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta, Rais wa Rwanda, Paul Kagame, Rais wa Uganda, Yoweri Museveni na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunzinza.
Waziri wa mambo ya Nje ,Uhusiano wa Afrika Mashariki,Balozi Dk Augustine Mahiga akisalimiana na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Afrika Mashariki ,Dkt. A.M Kirunda Kivejinja katika mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
Mawaziri mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
Mawaziri mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
Mawaziri mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo
Mawaziri mbalimbali wa Jumuia ya Afrika Mashariki waliohudhuria Mkutano huo. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii