Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117186

UWAPO MJINI MOSHI MAMBO YOTE UTAYAPATA EAST POINT HOTEL

$
0
0
Je, wajua kwamba Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine?  Basi kaa chonjo ufahamishwe!
Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame). Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. 
Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabila mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha. 
Usipate shida ndugu yangu. Ukitaka kujua mengi zaidi juu ya Wachagga, ama kupanda Mlima Kilimanjaro, ama kutembelea mbuga za wanyama za Kaskazini, tembelea MOSHI ambao unasifika nchini kuwa ni mji msafi kuliko yote. 
Na unapokuwa hapo fikia EASTPOINT HOTTEL iliyopo kona ya mitaa ya Swahili na Liwali katikati ya mji wa Moshi. Ni hoteli mpya na ya kisasa inayoongoza kwa huduma bora na mandhari nzuri za Mlima Kilimanjaro.



Viewing all articles
Browse latest Browse all 117186

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>