Wakwanza ni muhamasishaji wa huduma ya Airtel Yatosha aliyevalia kijamii ya maasai Bw Petro Abraham Lucas akiwa na Wafanyakazi wa Airtel wakiwa wameshikana mikono kama ilivyo katika tangazo lao la gazeti na televisheni kuashiria kuwa huduma ya Airtel Yatosha kifurushi cha SIKU imeboreshwa na sasa ni masaa 25, ishara hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye barabara ya Ali Hassan Mwinyi.
Mkuu wa kitengo cha Biashara mpya cha Airtel Bw, Godfrey Mugambi akiwa na wafanyakazi wenzake wakiwa wameshikana mikono kuonyesha kweli Airtel Yatosha.
Wafanyakazi wa Airtel Tanzania makao makuu Dar es salaam wakiingia barabarani huku wameshikana mikono kwa maandamano ikiwa ni tukio maalum la kuitambulisha TOSHA 24+1=25.
Kikundi cha Airtel yatosha kikitoa burudani katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi wakati ambapo wafanyakazi wote wa Airtel jijini Dar e salaam waliposhikana mikono kuashiria kuboreshwa kwa huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga. Ili mteja kujiunga anatakiwa kupiga *149*99# , tukio hili lilifanyika mwishoni mwa wiki katika barabara hiyo.
Wafanyakazi wa Airtel toka vitengo mbalimbali wakiwa wamejipanga na kushikana mikono kuashiria kuboreshwa kwa huduma yao ya Airtel Yatosha kwa wateja ambayo sasa imeboreshwa zaidi ili kumuongezea mteja muda zaidi wa kutumia kifurushi chake cha siku kwa masaa 25 toka alipojiunga. Ili mteja kujiunga anatakiwa kupiga *149*99# , tukio hili lilifanyika mwishoni mwa wiki katika barabara ya Ali Hassan Mwinyi,jijini Dar.