Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

KIGAMBONI YAONGEZA WIKI MOJA YA UUZAJI WA VIWANJA

$
0
0
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

 MKURUGENZI Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni,Stephen Katemba amesema kuwa mji wa kigamboni utajengwa kwa kisasa na kuwataka wananchi kwenda kup[ata viwanja vilivyopimwa.

 Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake, Katemba amesema kuwa walitangaza utoaji wa fomu za wananchi wanaotaka viwanja katika mji wa Kigamboni kuanzia ni Aprili 18 hadi 25 mwaka huu na utoaji wa fomu hizo unaendelea hadi Mei 2 pamoja na siku zote huduma zitatolewa bila kujali mapumziko na siku kuu. 

 Katemba amesema wameanza katika viwanja 6000 kwa awamu ya kwanza na wataendelea na awamu zingime lengo ni kutaka mji huo kuwa wa kisasa kuliko mji mingine iliyoo katika jiji la Dar es Salaam. 

 Amesema viwanja hivyo viko katika maeneo ya Kisarawe, Somangila, Ukooni ambapo wananchi watakao kuwa na viwanja hivyo watapata hati na malipo yake yanatakiwa ndani ya miezi miwili baada ya kurudisha fomu hizo. Aidha amesema wale wote watakaorudisha fomu hizo na kulipa ni uhakika kupata viwanja hivyo hakuna utapeli katika viwanja vya Kigamboni. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akizungumza na waandishi habari (hawapo pichani)juu ya Uuzaji wa viwanja katika Mji wa Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akionyesha Ramani kwa waandishi habari maeneo ambayo viwanja vinauzwa katika awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni, Stephen Katemba akitoa maelekezo kwa wananchi waliofika katika kupata huduma za viwanja leo jijini Dar es Salaam.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>