Msemaji wa Simba Haji Sunday Manara amefungiwa kutojihusisha na mchezo wa soka kwa muda wa miezi 12 na kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni tisa , kwa utovu wa nidhamu wa kutoa matamshi yasiyo na staha kwa viongozi wa TFF pamoja na vyombo vya uongozi wa mchezo huo. Makamu Mwenyekiti wa kamati ya nidhamu ya TFF Wakili msomi Jerome Msemwa pia amesema Haji Manara anaweza kukata rufaa.
↧