Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Dkt. Omary Chillo (kulia) akifafanua jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za HEART MARATHON na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika, jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu na kushoto ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John. Mbio hizo zitaanzia na kuishia barabara ya Kaole Oysterbay jijini Dar es salaam. Muda wa kuanza ni saa 12 asubuhi.
Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara akizungumza na wandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika jijini Dar es Salaam, kulia ni Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John.
Katibu Mkuu wa Taasisi ya Tanzania Health Summit Bi. Rebecca John (katikati) akisisitiza jambo kwa wandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea maandalizi ya mbio za heart marathon na upimaji wa afya yenye lengo la kuisaidia serikali kupunguza magonjwa yasiyoambukizika, jana jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Chama cha Riadha Tanzania Bi. Ombeni Zavara na kulia ni Katibu Mkuu Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Lucas Nkungu.