Serikali ya Awamu ya Tano iko katika mkakati wake kabambe wa kuhakikisha kuwa Sera ya Tanzania yenye viwanda inafanikiwa, lengo kubwa likiwa ni kukuza na kuinua uchumi wa nchi.
Yote hayo yanafanyika kwa kufufua viwanda mbalimbali ambavyo vilikuwa vimekufa na kusitisha uzalishaji wake kutokana na sababu mbalimbali hatua inayokwenda sanjari na kujenga vipya.
Tunashuhudia juhudi kubwa za Serikali zikizaa matunda katika maeneo kadhaa ya taifa letu ambayo tayari wawekezaji wameanzisha viwanda vya kutengeneza bidhaa mbalimbali.
Katika kudhihirisha hilo, pia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji inayoongozwa na Waziri Charles Mwijage imejikita katika kuwezesha wajasiriamali ili wainuke na kutambulika katika soko la kitaifa na kimataifa.
Hilo linafanyika kupitia maonesho mbalimbali ya viwanda na biashara ambayo hufanyika kila mwaka lengo ni kuwapa fursa wajasiriamali hao kuonesha bidhaa zao haijalishi kama ni kubwa au ndogondogo. Katika hilo Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu iliyopo katika Mkoa wa Shinyanga magharibi mwa Tanzania haiko nyuma kwani tayari imeanza utekelezaji wa sera hiyo muhimu kwa ustawi wa nchi.
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Nyabaganga Taraba akizungumza katika moja ya vikao. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya hiyo, Stephen Magoiga na Mwanasheria wa wilaya, Wilson Nyamunda.
Mmoja wa mafundi wa bidhaa za ngozi katika kiwanda kidogo cha Badimi akiwajibika.
Sehemu ya mifugo ambayo ni muhimu kwa uwekezaji wa viwanda vya bidhaa za ngozi wilayani Kishapu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA