Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Augustino Mrema amesema kuna changamoto nyingi sana katika kuendesha bodi hiyo na kumuomba Rais Dr John Pombe Magufuli kumwezesha ili atimize majukumu yake.
Akizungumza kupitia kipindi maalum cha Radio UFM (ya Azm Tv),Mrema amesema kuwa anaiomba serikali kuiangalia upya bodi hiyo kuhusu hali ya wafungwa nchini na mchakato wa kuwatoa wafungwa walio katika hatua za kisheria za Parole.
Mrema amesema , anaukumbusha umma kuwa kila mtu ni mfungwa mtarajiwa na serikali haiwezi kufanya mambo yote hivyo watanzania wakiwa na utamaduni wa kuyasaidia magereza yetu itasaidia kupata angalau virago kwa ajili ya wafungwa. Aliongeza kuwa utaratibu wa Parole ni mchakato unaohitaji gharama hivyo bodi yake inajitahidi kupata fedha ili kufanikisha majukumu yao.
Akizungumzia hali ya kisiasa nchini, Mrema amesema kuwa viongozi waliopo madarakani na wale waliomaliza muda wao kufanya kazi pamoja na Rais ikiwemo na kumpa ushauri utakaojenga nchini na sio kumbeza kama watu wanavyofanya.
Watanzania waache kukosoa kazi za Rais na kuacha kuandika mabaya yake kwani siku hizi mtu akiongelea kitu kibaya ndite anaonekana anafaaa lakini kitu hicho kinajenga taswira mbaya na zaidi hata katika Kumbukumbu ya Mwalimu Julius Nyerere aliongea mambo mazito lakini hakuna chombo cha habari kilichoandika.
Mrema amesema, katika wazalendo wa nchi hii yeye ni mmoja wao kwani anafanya kazi hiyo pasipo kujali mshahara ama posho yoyote pia alitumia nafasi hiyo kumuomba radhi Rais mstaafu wa awamu ya tatu Mhe Benjamini William Mkapa kwa makosa aliyowahi kumfanyia katika kipindi chake kwa kumsingizia kuwa aliiba Tshs Milioni 900, akasema ule ulikuwa ni mpango wa makusudi ingawa walipoenda mahakamani alishinda.