Baadhi ya wadau wanaosaidia kufanikiwa kwa Tamasha la Nyanza Festival 2017 ni SBL-Pepsi, Delta Media Studios, Kali Boy Music, Lake Fm, Passion Fm, Metro Fm, City F, Barmedas Tv, Binagi Blog-BMG, Tanzania Bloggers Network-TBN na Tamara Entertainment.
BMGHabari
Hatimaye uongozi wa Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza, umethibitisha kwamba tamasha la burudani la Nyanza Festival 2017 litafanyika katika uwanja huo kama ilivyokusudiwa.
Meneja wa uwanja huo, Steven Shija, ameyathibitisha hayo baada ya kutokea figisu figisu kwamba siku ya tamasha hilo kutakuwa na mchezo wa soka wa Ligi Kuu nchini na hivyo kusababisha tamasha hilo kutofanyika.
"Ndugu Wasanii na Waandaaji wa Nyanza Festival napenda kuwajulisha kuwa ratiba ya Tamasha ipo pale pale hakuna kitakachoiathiri, tunasimamia utaratibu na misingi ya haki kwa tunaowahudumia. Nawatakia maandalizi mema ya Tamasha lenu". Amebainisha Shija.
Tamasha la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika Jijini Mwanza la Nyanza Festival 2017, litafanyika wikendi hii April 15 na 16 kwa kiingilio cha 5,000 tu ambapo wasanii zaidi ya 30 watapanda jukwaani.
Kumbuka Nyanza Festival ni tamasha lililoasisiwa na Wanatasnia mbalimbali kutoka Kanda ya Ziwa wakiwemo wanamuziki, watangazaji, waandishi wa habari, Madjz na wadau wengine wengi kupitia umoja wao wa Mwanza.Com chini ya kampuni ya Famara Entertainment, lengo likiwa ni kuukuza na kuuendeleza zaidi muziki wa Kanda ya Ziwa.