Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wazee Vijana Wanawake na Watoto Zanzibar Mhe Maudline Cyrus Castico akizungumza wakati wa kufunga kongamano la Vijana barani Afrika lililoandaliwa na Taasisi ya Unogozi Instute na kuwakutanisha vijana zaidi ya 45 ambao walipata muda wa kukaa na kujadili mustakabali wa maendeleo ya bara la Afrika.
aidha Mh. Castico amewaasa wa Vijana kuacha kukata tamaa na maisha na kujiwekea imani ya kuwa wao ndio viongozi wa Mataifa haya ya Afrika na kuwaomba kuendeleza umoja wetu ambao umeachwa na wasisi ambao walipigania uhuru.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Insitute, Profesa Joseph Semboja akizungumza kabla ya kumakaribisha mgeni rasmi kufunga warsha hiyo ya Vijana Afrika.
Baadhi ya washiriki wakifurahi mara baada ya kusikiliza maneno mazuri kutoka kwa mgeni rasmi
Vijana wakinyoosha mikono juu kama ishara ya umoja wao katika maendeleo ya Bara la Afrika