Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 117069

Rais Mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete Akutana na Rais Dennis Sassou Nguesso wa Congo Brazaville

$
0
0
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  ( Education Commission on Financing Global Education Opportunity) juzi tarehe 21 Machi, 2017, amekutana na Rais wa Jamhuri ya Congo Mhe. Dennis Sassou Nguesso alipomtembelea Ikulu yake jijini Brazaville.
Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi  Rais Sassou Nguesso Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja  (miaka 30). 
Azma kuu ya Mpango huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanapata elimu iliyo sawa, na kwa kiwango cha ubora unaolingana dunia nzima.
 Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  ( Education Commission on Financing Global Education Opportunity) akilakiwa na  Rais wa Jamhuri ya Congo Mhe. Dennis Sassou Nguesso alipomtembelea Ikulu yake jijini Brazaville.
  Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  ( Education Commission on Financing Global Education Opportunity) akimkabidhi ripoti hiyo  Rais wa Jamhuri ya Congo Mhe. Dennis Sassou Nguesso alipomtembelea Ikulu yake jijini Brazaville.
 Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Kupendekeza Namna Bora ya Kugharamia Fursa ya  Elimu  Duniani  ( Education Commission on Financing Global Education Opportunity)akiongea na wanahabari  jijini Brazaville. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Viewing all articles
Browse latest Browse all 117069

Trending Articles