Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akiandika kwenye daftari la mwananfunzi aliyekaa pembeni yake kama ishara ya matumizi ya madawati 320 yaliyokabidhiwa na taasisi ya Hassan Maajar Trust ya jijini Dar es Salaam tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense ikiwa ni jitihada za taasisi hiyo kusaidia elimu nchini. Mkuu huyo wa Mkoa aliishukuru taasisi hiyo na kusema mfano wake ni wa kuigwa ukilinganisha na taasisi zingine ambazo huishia kuilamu Serikali na huduma zilizopo badala ya kutoa mchango wowote. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hassan Maajar Trust Bi Zena Tenga na Makamu Mwenyekiti Ndugu Shariff Maajar. Wa tatu kutoka kushoto aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akimkabidhi Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar shilingi laki moja na nusu ili aikabidhi kwa mwalimu mkuu shule ya msingi Kasense ikiwa ni sehemu ya azimio alilolianzisha na kuliita "Azimio la Kasense" KADARU (Kampeni ya Dawati Rukwa) katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi ya Hassan Maajar Trust kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013.
Makamu Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bw. Shariff Maajar akizungumza katika hafla fupi kukabidhi madawati 320 ya taasisi hiyo kwa shule za msingi Mkoani Rukwa tarehe 06-06-2013 katika shule ya msingi Kasense, Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima, Meya Manispaa ya Sumbawanga Sabas Katepa na Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Bi. Zena Tenga.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI