Ewe mshabiki wa muziki wa dansi wa hapa nyumbani uliotamba katika miaka ya sabini hadi tisini, usikose kujivinjari katika ukumbi wa maraha wa nyumbani lounge kila siku ya jumatano kuanzia saaa tatu usiku, ambapo Isaac Muyenjwa Gamba akishirikiana na mchambuzi wa muziki wa dansi Rajabu Zomboko, watakuletea disco la muziki huo pamoja na miondoko ya bakulutu, katika BAKULUTU NITE ndani ya nyumbani lounge.
Njoo wewe na yule upate zile za Dar International, maquiz du zaire, ochestra safari sound, sikinde ngoma ya ukae , msondo ngoma nk, bila kusahau za francoo luambo makiadi, tabuley, sam mangwana na bibie mbilia bell live ambazo hazijachakachuliwa. Pichani Isaac Muyenjwa Gamba akiwa mitamboni ndani ya club ya numbani lounge akiwapagawisha vijana wa zamani.