Salaam Ankal
Kwa kweli wajumbe wa tume ya katiba wameyatendea haki maoni ya watanzania juu ya katiba mpya. Ingawa sijapata muda wa kusoma kifungu hata kifungu kwa utulivu, lakini kwa muonekano wa awali rasimu ni nzuri na itahitaji marekebisho machache ya kimsingi.
Rasimu ya katiba imependekeza kuwepo kwa serikali tatu, yaani ya Muungano, ya Tanzania zanzibar(ambayo ipo kwa sasa) na ya Tanzania Bara( ambayo katika katiba ya zamani imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania). Kwa utaratibu wa tume rasimu ya katiba itajadiliwa katika mabaraza mbalimbali yalioundwa katika ngazi tofauti na baadae kwenye bunge la katiba na mwishowe itapigiwa kura ya maoni na itakuwa tayari mwaka 2014. Serikali , inataka katiba hii ianze kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Angalizo langu:
Iwapo katiba hii itapita katika mchakato mzima na ikakubalika kwa wananchi kwamba tuwe na serikali tatu. Serikali ya Muungano itakuwa na katiba, Serikali ya Tanzania Zanzibar wanayo katiba yao, Serikaliya Tanzania bara itakuwa haina katiba yake, hivyo basi tutabidi tuanze mchakato mpya wa kupata katiba ya serikali ya Tanzania bara mwaka 2014. Hili linaweza kuchukua muda mrefu na pengine kuchelewesha au kuhairisha uchaguzi wa mwaka 2015.
Sijui serikali na wanasiasa wanaliangaliaje hili.
Wadau wa blog je mna mawazo gani kuhusu angalizo hili?