Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

kinana na ujumbe wake wa ccm awasili mkoani njombe leo,kufanya ziara ya siku saba mkoani humo, awaonya wanaojipitishapitisha kutaka urais

$
0
0
NA BASHIIR NKOROMO, IRINGA 
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana amesisitiza kwamba Chama kitamwadhibu bila huruma mwanachama yeyote anayejipitisha-pitisha katika maeneo mbalimbali na kufanya kampeni za kuwania urais kabla ya wakati.
 Kinana alisema hayo leo wakati akizungumza na Kamati ya Siasa na mkoa wa Iringa, katika kikao maalum, kilichofanyika kabla ya kwenda mkoani Njombe ambako ameanza ziara ya siku saba mkoani humo. 
 Kinana alisema, katazo la wanachama kujipitisha-pitisha na kupiga kampeni za kuwania urais au nafasi yoyote kabla ya muda halitoki midomoni mwa viongozi bali ni kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Chama. "Ndugu zanguni, nawakumbusha kwamba kwa hili hatuna mzaha nalo, hivyo hakikisheni kila mmoja wenu kama kiongozi hajihusishi kwa namna yoyote kushiriki katika kutumiwa na wanachama hao wanaojipitishajiptisha", alisema Kinana na kuongeza; 
 "Ni lazima Chama kiwe kikali kwenye jambo hili, kwa sababu kama kitawaacha watu hawa kukiuka taratibu na kanunzi za Chama wanazidi kukifanya chama kuwa na makundi mengi ambayo yatakipeleka pabaya," alisema Kinana Kinana alisema, kazi walioyonayo wale wote wanaokitakia mema Chama, ni kumuunga mkono Mwenyekiti, Rais Jakaya katika kazi ya kuhakikisha CCM inakamilisha utekelezaji ilani yake ya Uchaguzi kwa kiwango kinachostahili na siyo muda kujipitisha pitisha mtu binaafsi kwa wanachama huku utekelezaji wa ilani ukisinzia. 
 Alisema kuwa hivi sasa kazi ya CCM ni kuhakikisha inatekeleza ilani ya uchaguzi kwa kipindi kilichobaki cha miaka miwili ya nusu kabla ya kumalizi kwa awamu ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete.
 "Ni wazi kazi yatu CCM ni kuhakikisha tunatekeleza ilani ya uchaguzi kwa vitendo na si mamneno kama wanavyofanya wengine. ni kazi kubwa imefanyika chini ya uongozi wa Rais Kikwete na katika kipindi cha miaka miwili iliyobaki tumedhamiria kuifanya zaidi"
Alisema moja ya maeneo ambayo licha ya kuwepo changamoto za hapa na pele lakini yamefanikisha sana utekelezaji wa ilani ya CCM, ni kwenye Halmashauri mbalimbali nchini ambapo watendaji walio wengi wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi. 
 "Kwa kweli CCM lazima hawa tuwapongeze maana kuna wengine kazi yao imebaki kuwashambulia huku wakijua watendaji hao hawana fursa ya kujitete mbele ya jamii. chapeni kazi nasi tupo nyuma yenu, na kila wakati tutakuwa tukitambua juhudi na kazi kubwa mnayoifanya kwa jamii," alisema Kinana. 
 Akizungumzia uchaguzi mdogo wa madini unaofanyika katika kata mbalimbali nchini Kinana, alisema CCM itashinda uchaguzi huo kwenye kata zote 25 kutokana na mtandao wa chama chake na imani inayoonekana kuwepo kwa wananchi juu ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akilakiwa na Mbunge wa Njombe Kaskazini,Mh Deo Sanga a.k.a Jah People mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akivalishwa skafu .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa jimbo la Ludewa,Mh.Deo Filikunjombe,kushoto shati la drafti ni Mbunge wa jimbo la Mwibara,Mh Kange Rugora

Pichani kulia ni Mjumbe wa kamati kuu na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Njombe,Pindi Chana akicheza na akina mama wakati wa mapokezi ya katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana 
 Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye  akishirikiana na  mmoja wa wapiga ngoma za asili wakati walipowasili leo mapema mchana wakiongozwa na  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana
 Ndugu Kinana na ujumbe wake wakipokelewa kwa shangwe mapema jionu ya leo,mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye .
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akitazama moja ya kikundi cha ngoma kilichofika kumlaki,mara baada ya kuwasili jioni ya leo mpakani mwa Mkoa wa Iringa na Njombe katika kijiji cha Idofi,kata ya Mlowa,ambapo pia alipokelewa na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Njombe akitokea Mkoani Iringa ambaka aliwasili leo Asubuhi akitokea jijini Dar akiwa ameambatana na Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Ndugu Nape Nnauye.

Ndugu Kinana na ujumbe wake watakuwa na ziara ya siku saba mkoani Njombe ambapo watatembele Wilaya zote za Njombe,Makete, Ludewa na Wanging'ombe  wakiimarisha chama na kusikiliza matatizo ya Wananchi,huku wakikagua miradi ya maendeleo mbalimbali katika kusimamia serikali ili kutekeleza Ilani uchaguzi ya CCM.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>