Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

WAKUU WA JESHI LA MAGEREZA NCHINI NAMIBIA NA TANZANIA WASAINI MAKUBALIANO YA KUTOA MAFUNZO KWA MAAFISA WA JESHI LA MAGEREZA NAMIBIA

$
0
0
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akipongezana na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo baada ya kusaini makubaliano ya kutoa mafunzo kwa maafisa wa Jeshi la Magereza wa nchini Namibia. Tukio hilo lilishuhudiwa na maafisa mbalimbali wa majeshi hayo. Makubaliano hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa kwa ajili yake katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo akiijaribu moja ya silaha inayotumika kwa ajili ya kutuliza ghasia wakati wowote inapotokea ndani na nje ya gereza. Shikongo alionyweshwa silaha mbalimbali ambazo zinatumika kwa ulinzi na kutuliza ghasia Magerezani katika maonyesho yaliyoandaliwa kwa ajili yake na Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia cha Jeshi la Magereza, Ukonga Dar es Salaam.
Askari wa Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, wakimuonesha mbinu za kupambana na adui pasipo kutumia silaha Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo (hayupo pichani) pamoja na makamishna wengine wa jeshi hilo ambao walitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ya Jeshi hilo, Ukonga jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga, ACP Mbaraka Semwanza akitoa taarifa fupi ya chuo hicho kwa Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Kamishna Jenerali Evaristus Shikongo (katikati). Kushoto aliyekaa ni Kamishna wa Sheria na Utawala wa Jeshi la Magereza, Dk Juma Malewa, kulia ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga, anayefuata ni Kamishna wa Rasilimali Watu, Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza nchini Namibia, Clementine Feris. Picha na Felix Mwagara.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles