Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

KILWA YAPITISHA MPANGO WA AMANI NA MAENDELEO

$
0
0
Jengo la Ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Mh. Abdalah Ulega akizungumza na wadau waliokutana leo kwa ajili ya kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.
Baadhi ya Wadau waliohudhulia mkutano huo.


Na Abdulaziz video-kilwa

Serikali wilayani Kilwa imetakiwa kuwa na uwazi katika fursa mbalimbali za maendeleo kwa kushirikisha jamii ili kufanikisha wilaya hiyo kuinuka kiuchumi kupitia Raslimali zilizopo Wilayani humo.

Hayo yameelezwa na baadhi ya wadau waliokutana leo kwa ajili ya kujadili Amani na Maendeleo ya Wilaya hiyo kufuatia machafuko yanayoendelea hivi sasa mikoa ya Kusini kutokana na Kutokuwepo Ushirikishwaji baina ya watendaji wa Serikali na Jamii hali inayochangia jamii nyingi Nchini Kukosa Imani na Serikali yao.

Wakichangia katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa PEC wilayani humo na kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, siasa ,asasi za jamii na watendaji wa serikali waliokutana katika kikao kilichoitishwa na Mkuu wa wilaya hiyo,Abdalah Ulega kimelenga kuzungumzia hali ya amani ,usalama na maendeleo ya kilwa ambapo alitoa fursa kwa wananchi hao kujadili kwa undani na kuweka mikakati ya kuhakikisha Amani Inadumishwa ndani ya wilaya hiyo na Mkoa.

Awali akitoa taarifa ya Mapato ya mrahaba wa Gesi asilia ya Songo Songo kwa Wilaya,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo,Addoh Mapunda alibainisha kuwa licha ya wananchi wanaoishi eneo la Songosongo kunufaika na gesi inayopatikana kwenye kijiji cha Songosongo alieleza Kuwa Madiwani wa Halmashauri hiyo wamepitisha 35% ya malipo ya mrahaba huo wa gesi utumike katika kuboresha elimu Nae Mkuu wa Wilaya Hiyo,Abdallah Ulega aliwasihi wananchi wa Wilaya hiyo kujipanga na Kushirikiana na Serikali yao kudumisha Amani ikiwa pamoja na kufungua fursa kwa Wananchi kueleza changamoto na kero mbalimbali walizonazo kabla hawaichukia Serikali kutokana na Ushawishi wa Dini na Siasa ikiwemo na Mataifa mbalimbali.

Kufuatia uwepo wa Gesi asilia ya Songosongo wilaya ya Kilwa upata mrahaba wa Mil 100 kwa Mwezi ambapo asilimia 35 hutumika katika kuboresha Elimu,Asilimia 20 kijiji cha Songosongo huku 45% zikichangia katika shughuli za maendeleo wilayani humo.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>