Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

WARSHA YA WAZI KUJADILI MATOKEO YA UCHAMBUZI WA KINA WA MAENEO YA KIPAUMBELE YA KITAIFA

$
0
0
Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi (Ikulu) inawatangazia na kuwaalika wadau na wananchi wote kuhudhuria Warsha ya Wazi (Open Day) kupata maelezo, kujadili na kutoa maoni juu ya miradi na program zitakazotekelezwa na Serikali kwa kipindi cha miaka mitatu (2013/14 hadi 2015/16) katika maeneo ya kipaumbele yaliyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12-2015/16). 
Miradi hiyo inatokana na uchambuzi wa kina uliofanywa na wataalamu wa kitanzania kwa kutumia mfumo mpya wa kimaabara (labs).
Huu ni mfumo ambao Serikali imeuanzisha ili kuhakikisha ushirikishwaji mpana wa wadau na wananchi kwa ujumla katika utekelezeaji wa miradi ya kipaumbele ya Kitaifa.
Warsha hiyo ya wazi itafanyika kesho Ijumaa tarehe 24/05/2013 katika viwanja vya Makumbusho ya Taifa mkabala na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar Es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Wote mnakaribishwa!
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano
Ikulu
DAR ES SALAAM

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115279

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>