Mkutano wa Internet Forum unaendelea mjini Stockholm kwa siku ya pili, ukijadili mambo muhimu kama upatikanaji wa mtandao kwa watu wote na kwa gharama nafuu (Free access for all) na jinsi ya kuchochea maendeleo ya ubunifu na kutengeneza programu na vifaa vya TEHAMA (Accerelating innovations in ICT for transformative growth)ambayo wananchi wengi watakuwa wana uwezo wa kuvipata na kuvimiliki.
Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa wa sweden Bi. Gunilla Carlsson akifafanua jinsi gani Mtandao unaweza kutumika katika kuwaletea maemaendeleo wananchi.
Panelist ikijadili “Accerelating innovations in ICT for transformative growth”.
Waziri wa Technologia ya Mawasiliano na Habari wa Sweden Bi. Anna-Karin Hatt, Professor Paula Uimonen, Director of SPIDER wakizungumza na Bw. Wilfred warioba, kutoka Tume ya Haki za Binadamu na Dr. Jabiri Bakari CEO wa Tanzania e-Governance Tanzania.