Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

OPARESHENI YA POLISI MORO KUSAKA WAHARIFU NA WAPIKAJI WA POMBE HARAMU YA GONGO

$
0
0
JESHI la Polisi Mkoani Morogoro limefanya msako mkali katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Morogoro na wilaya ngingine za Mkoa huo na kufanikiwa kuwatia mbaroni watu zaidi ya 33 wakituhumiwa kufanya makosa ya uharifu na utengenezaji wa pombe haramu ya gongo na usafisishaji wa bangi.

Askari Polisi wakiongozwa na Makamada kuanzia mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, walifanya msako huo walianzisha msako huo katika maeneo ya Kata ya Lukobe, Kingolwira na maeneo mengine na kufanikiwa kukamata pombe haramu ya gongo lita 600, mitambo 22 , vyombo vya kupikia 124 , madumu 60 na magunia manene ya bangi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongike , alisema hayo Mei 22, mwaka huu alipozungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake na kuwaonesha vitu hiyo vilivyowekewa eneo la viwanja vya Ofisi ya Polisi Mkoa.

Hata hivyo alisema katika opareshani hiyo , Polisi imefanikisha kukamatwa kwa meno vipande 320 vya Kiboko na meingine mawili ya Nyati katika Wilaya ya Kilombero.

Katika hatua nyingine Polisi imefanikiwa kumtia mbaroni askari wa zamani mwenye cheo cha Koplo Usu Omari Abdallah ambaye alifukuzwa a uaskari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) Kikosi cha Ruvu, Mkoani Pwani baada ya kukutwa akiwa na sare ya Jeshi hilo.

Hatua ya kukamatwa kwake ilitokana na taarifa ya raima mwema na kwamba mtuhumwa alikuwa akiishi eneo la Msamvu , Manispaa ya Morogoro

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, askari hiyo wa zamani wa JWTZ licha ya kufukuzwa kazi aliendelea kubaki na sare za Jeshi hilo ‘ combati’ kinyume na sheria za Majeshi na kuitumia katika kufanya uharifu wa kutampeli wananchi.

Hata hivyo Kamaanda huyo wa Mkoa , alisema Opereshani hiyo ni endelevu na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano ili kutokomeza mambo hayo ya kiharifu mkoani Morogoro.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile ( mwenye fimbo) akiangalia mifuko ya mbolea iliyobadirishwa kwa baadhi kuwekwa mbolea Minjingu katika mifuko ya mbolea yenye nembo ya aina ya CAN baada ya kuikamata hivi karibuni katika ghala la mfanyabiashara wa Duka la Pembejeo za kilimo eneo la Nane Nane , Mjini Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile akiwaonesha Waandishi wa Habari ( hawapo pichani) baadhi ya vitu vya aina mbalimbali ikiwemo mitambo ya kupinga pombe haramu ya gongo, mapipa , madumu na mifuko ya mbolea iliyochakachuliwa, viroba vya bangi na sare moja ya JWTZ ,ambayo kwa pamoja vilikamatwa na Polisi wakati wa oparesheni iliyioanza Mei mosi mwaka huu hadi Mei 22, mwaka huu mkoani Morogoro.
Baadhi ya Askaari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro walioshiriki oparesheni ya ukamataji wa mitambo na mapipa ya gongo.Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii,Morogoro.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>