Baadhi ya vijana wakiuliza maswali toka kwa wataalamu wa COSTECH juu ya Kazi na Mchango wa COSTECH katika elimu ya juu,Sayansi na Teknolojia katika Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es salaam.
Mfanyakazi wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,Frank Makalla(kushoto) akimuelezea mwanafunzi wa elimu ya Juu kuhusu jinsi COSTECH inavyohusika kuishauri serikali juu ya Mambo yote yanayohusu sayansi,Teknolojia na Ubunifu nchini.
Moja ya mwanafunzi aliyemaliza kidato cha Sita akipewa ufafanuzi kuhusu Sheria No 7 ya Bunge ya Mwaka 1986 iliyoiunda COSTECH na kulilithi lililokuwa Baraza la Taifa la Utafiti mwaka 1972.