Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi punde kutoka mkoani Mtwara,inaeleza kuwa kumezuka vurugu kubwa kati ya wananchi na Jeshi la polisi hali iliyopelekea Jeshi hilo kulazimika kutumia mabomu ya machozi kwa ajili ya kuwatawanya wananchi hao.
Chanzo cha vurugu hizo inadaiwa kuwa ni mara tu baada ya Bajeti ya Wizara ya Nishati na Madini kusomwa Bungeni na kueleza kuwa mradi wa gesi Mtwara utatekelezwa bila kutaja faida za moja kwa moja kwa wananchi hao.
Wananchi hao walianzisha vurugu leo huku wakiwa na kauli mbiu yao isemayo "Gesi haitoki hata kwa bomba la peni". Inaelezwa kuwa kuna kituo cha mafuta cha Total kimechomwa moto wakati wa vurugu hizo. Katika kukabiliana na vurugu hizo.
Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo na tutaendelea kupeana taarifa kadri zitakavyokuwa zikitufikia.