Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimkaribisha kwa mazungumzo Daktari bingwa wa watoto Jerome Paulson, Mkurugenzi wa Afya ya watoto na Mazingira kutoka Chidren's National Medical Center ya huko Washington nchini Marekani aliyemtembelea Mama Salma kwenye ofisi ya WAMA jijini Dar es Salaam tarehe 21.5.2013. Dr. Jerome amekuja Tanzania kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa Madaktari Bingwa wa watoto hapa nchini kuhusu afya ya mtoto na mazingira kufuatia makubaliano aliyoyafanya na Mama Salma wakati alipotembelea taasisi hiyo huko Washington mwaka 2012.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Daktari Bingwa wa watoto Jerome Paulson aliyeambatana na Mkewe pamoja na viongozi wa Chama cha Madaktari wa watoto hapa Tanzania (Paediatrc Association of Tanzania-PAT). Kutoka kushoto ni Dr. Augustino Masawe akifuatiwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa watoto nchini (PAT) Dr. Rodrick Kisenge, Mrs Jerome na kwa nyuma ni Dr. Francis Furia,Mjumbe na Dr. Hadija Mwamtemi, Mwekahazina wa chama hicho.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Daktari Bingwa wa Watoto Jerome Paulson kutoka Marekani na Viongozi wa Chama cha Madaktari wa Watoto hapa Tanzania kwenye ukumbi wa mikutano wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, tarehe 21.5.2013. PICHA NA JOHN LUKUWI