Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Majaliwa awataka wanasiasa kuacha uchochezi katika jamii

$
0
0
Na Abdulaziz Video,Lindi 
 Naibu waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa [TAMISEMI] Mhe Kassim Majaliwa ambaye pia ni mbunge wa Ruangwa amewataka wanasiasa mkoani Lindi kuacha tabia ya kuwa chanzo cha kuchochea vurugu katika jamii badala yake washirikiane na watendaji na wananchi ili kuinua mkoa huo ambao huko nyuma kimaendeleo. 
Naibu waziri huyo ametoa wito huo wakati alipokuwa anazungumza na wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri mkoa [RCC] katika ukumbi wa mkuu wa mkoa Lindi.
Alisema kazi kubwa ya wanasiasa ni kutembelea wananchi kwa lengo la kuwasikiliza kero zao ,kuwahimiza na kuwahamasisha wananchi katika maeneo yao ili kuchochea maendeleo na sio kuchochea kufanya vurugu na kusababisha kuvunjika kwa amani. 
"Wanasiasa wamekuwa na nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko chanya katika maeneo yao kwa kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za maendeleo badala ya kushiriki vurugu.
“Sio vyema wanasiasa waliochaguliwa na wananchi kwa ajili ya kusimamia na kuwawakilisha wakatumia nafasi hiyo majukwaani kutamka maneno ya uchochezi na kusababisha kupotea mwelekeo wa kuwaletea wananchi wake maendeleo hii inaonesha usivyotosha kwa wapiga kura", alimalizia Mhe Majaliwa 




Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara
Wenyeviti wa Halmashauri za mkoa wa Lindi wasikiliza kwa makini kikao cha Bodi ya Barabara

Naibu Waziri wa Nchi Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa ambae Pia ni ,Mbunge wa jimbo la Ruangwa, Mhe Kassim Majaliwa, akibadilishana mawazo na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Dkt.  Nassor Ally Hamid wakati wa mapumziko mafupi ya Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Lindi
Mkuu wa Mkoa wa Lindi,Mhe Ludovick Mwananzila akifunga kikao cha bodi ya Barabara Mkoa

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>