Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

waziri mkuu pinda apokea matembezi ya mshikamano ya kupapambana na maharamia wa kazi za sanaa mjini dodoma leo.

$
0
0

Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na na baadhi ya Watangazaji wa Clouds FM (wote waliosimama nyuma).Reedio Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa TWENZETU  kwa minajili ya kuielimisha jamii  kuwa na tabia ya kupenda vya kwao na  kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA kujikwamua kimaisha.

Waziri Mkuu Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasaniii (wote waliosimama nyuma),mara baada ya kuzungumza nao kuhusiana na mambo mbalimbali juu ya sanaa ya Tanzania na namna ya kupambana na maharamia wa kazi zao,ambapo pia redio ya Clouds FM imezindua msimu wake mpya ulioitwa Twenzetu kwa minajili ya kueilmisha jamii ya kupenda vya kwao kutumia fursa walizonazo ndani ya MADE IN TANZANIA . 

Waziri Mkuu Pinda akizungumza mbele ya  baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya/Filamu pamoja na watangazaji wa Clouds FM na wadau wengine wa sanaa waliojumuika kwa pamoja kwenye tukio hilo adhimu kabisa mapema leo mchana,mara baada kufanyika Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini.

Mh.Pinda aliishukuru kampuni ya Clouds Media Group kwa kazi nzuri walioianzisha ya kuwasaidia vijana kwa namna moja ama nyingine katika suala zima la kuwaamsha na kuwafungua macho na kuwaelimisha namna ya kuziona fursa zilizopo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha,aliongeza  kuwa kupitia ujumbe huo wa MADE IN TANZANIA kinachohitajika sasa ni kupanga ratiba nzuri ya kuliendeleza zoezi hilo ikiwemo pia kwa kuzishirikisha taasisi nyingine zikiwemo za serikali katika kuhakikisha jambo hilo linaendelea.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Dkt.Rehema Nchimbi akiwakaribisha watu wote waliofika kwenye viwanja vya Nyerere Skwea,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Waziri Mkuu Pinda.
Baadhi Wadau wa Muziki na Filamu wakiwa na mabango yao yaliyobeba jumbe mbalimbali mapema leo kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
Sehemu ya umati wa watu ukiwa kwenye Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo na pia kuendelea kuutanua wigo wa upatikanaji wa fursa hizo kwa wasanii na vijana wenyewe katika nafasi ya kujikwamua kimaisha,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini,yaliyoanzia kwenye uwanja wa Jamhuri na kufikia tamati viwanja vya Nyerere Skwea 
 Baadhi ya Wasanii wa Filamu hapa nchini Wema Sepetu sambamba na shosti yake Kajala walikuwa ni miongoni mwa wasaani waliounga mkono matembezi hayo ya mshikamano yaliyokuwa yametawaliwa pia na mabango kadhaa yaliyobeba jumbe mbalimbali za kupinga wizi wa kazi sanaa.
 Matembezi ya mshikamano ya kuitaka Serikali iendelee kuzilinda fursa zilizopo,ikiwa sambamba na kupinga uwizi/uharamia wa kazi za sanaa hapa nchini .
 Baadhi ya Watangazaji wa clouds FM,sambamba na wasanii wa muziki wa kizazi kipya/tasnia ya filamu na wadau wengine wa sanaa wakiwa wamejumuika kwa pamoja kwenye viwanja vya Nyerere Skwea mapema leo mchana,tayari kwa kumpokea mgeni rasmi,Mh Waziri Mkuu Pinda.
PICHA ZAIDI INGIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>