Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Mkutano mkubwa wa kikanda wa kilimo waanza Dar leo

$
0
0
TANZANIA ni mwenyeji wa Kongamano kubwa la siku tatu la kikanda wa kilimo wa muungano wa umoja wa vyama vya kilimo kusini mwa Afrika (SACAU)ambao unaanza leo jijini Dar es Salaam na kumalizika kesho kutwa.

Kongamano hilo litakaloangalia kwa undani swala la jinsi ya kuhudumia kifedha kilimo cha Afrika limeandaliwa na Baraza la Kilimo na Mifugo Tanzania (ACT) kwa kushirikiana na SACAU ambapo maandalizi yake yamekamilika.

Mkurugenzi Mtendaji wa ACT, Bi. Janet Bitegeko, aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa takribani washiriki 200 kutoka nchi 14 za kusini mwa Afrika pamoja na wawakilishi wa vyama vya wakulima kutoka maeneo mengine ya Afrika wamethibitisha ushiriki wao.

“Mkutano utaangalia ushirikiano kati ya SADC/COMESA/EAC katika maswala ya kilimo na mambo mengine ambayo yanalenga kuleta mapinduzi ya kilimo katika nchini husika,” Bi. Bitegeko alisema.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo, mkutano huo ambao unafanyika hapa nchini kwa mara ya kwanza hapa nchini moja ya mambo mengine utaangalia makisio ya mahitaji ya bidhaa za kilimo duniani na kuona fursa na tishio lake kwa wakulima.

Bi. Bitegeko aliongeza kuwa kongamano ambalo litakalokusanya wakulima toka sehemu mbalimbali Afrika litashuhudia kuzinduliwa kwa mradi wa majaribio wa kilimo wa SACAU hapa Tanzania.

“Mkutano utaangalia ushirika huo kwa undani, muundo wake na umuhimu wake kwa wakulima na biashara katika sekta hii ya kilimo,” alisema na kuongeza kuwa kongamano hilo linakuja na majibu thabiti ya jinsi ya kuinua kilimo hapa nchini, katika kanda na Afrika kwa ujumla.

Baada ya kongamano hilo, SACAU itafanya mkutano mkuu wake wa mwaka na kufanya uchaguzi wake. Kwa sasa, Tanzania inawakilishwa na Bw. Salum Shamte katika bodi ya SACAU.

“ washiriki wa mkutano/kongamano huo watafanya ziara kutembelea wakulima wilayani Bagamoyo mkoa wa Pwani,” Bi. Bitegeko alisema. ACT ni chama kinachounganisha wadau mbalimbali wa kilimo hapa nchini.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>