Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu huyo katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea,anaeshuhudia kulia ni Meneja uhusiano wa nje wa Vodacom Tanzania,Bw.Salum Mwalim.
Mkuu wa kitengo cha huduma za mtandao Vodacom Tanzania Bw.Andrew Lupembe,akiongea na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapambano , kuhusiana na masuala ya Usalama Barabarani katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga katika kutoa elimu kwa watoto wa shule hiyo na Uzuri zote za Sinza jijini Dares Salaam na kutoa msaada wa madafutari na vitabu mbalimbali vya kujisomea.
Mfanyakazi wa Vodacom Tanzania,Bi.Ena Mwangama,akimkabidhi kitabu cha sayansi mmoja wa wanafunzi wa shule ya Mapambano iliyopo Sinza jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi wa vodacom Tanzania,walipofika shuleni hapo kutoa elimu ya Usalama Barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani yaliyoanza Mei 6 hadi 12.kila mwaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania , wakiwafundisha wanafunzi wa shule ya msingi ya Mapambano ya jijini Dar es Salaam, baada ya kuwapa msaada wa vitambu vya sayansi ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) kutoa elimu kwa watoto wa shule za Uzuri na Mapambano zote za Sinza jijini Dares Salaam.
Meneja wa Vodacom anaye husika na masuala ya elimu Grece Lyon akimkabidhi mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi ya Uzuri Tandale jijini Dar es Salaam, Vitabu vya Sayansi wakati wa Maadhimisho ya wiki ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,ambapo wafanyakazi wa vodacom waliambatana na mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini).
Meneja Mawasiliano wa Vodacom Rukia Mtingwa akiwaongoza wanafunzi wa shule ya msingi ya Uzuri iliyopo Tandale jijini Dar es Salaam, kwenda kujifunza jinsi ya kutumia alama za barabarani ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Umoja wa Mataifa ya Nenda kwa Usalama Barabarani ambayo huadhimishwa Mei 6 hadi 12 ,kila mwaka .Wafanyakazi wa Vodacom waliambatana na Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania,Mohamed Mpinga (hayupo pichanini) Pia walitoa msaada wa vitu mbalimbali ikiwemo vitabu vya Sayansi.