Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki Dr. Eliezer Feleshi akitoa ufafanuzi wa jambo katika mkutano wa waandishi wa habari hawapo pichani Mei 10, jijini Dar es Salaam wakati walipokutana kwaajili ya kutoa maazimio ya mkutano wa siku 2, uliowakutanisha Wakurugenzi wa mashtaka wa Afrika Mashariki. Nchi zinazojumuisha shirikisho hilo ni kutokaTanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.
.Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa nchi za Afrika Mashariki Martin Ngoga (kushoto) akitoa taarifa ya maazimio ya mkutano wao wa siku 2 kwa waandishi wahabari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salam.pichani kutoka (kulia) Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Uganda , Richard Buteera, Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki Dkt. Eliezer Feleshi , akifuatiwa na Mwendesha Mashtaka kutoka Burundi , Valentine Bugorikunda.
Mwandishi wa habari wa magazeti ya kampuni ya TSN ya jijini Dar es Salaam , Abdlul Saliboko akiuliza suali katika majumuisha ya mkutano wa siku mbili wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka Afrika Mashariki.
Baadhi ya Washiriki wakifuatilia hotuba ya Rais wa Shirikisho la Wakurugenzi wa Mashtaka wa Afrika Mashariki Martini Ngoga kutoka Rwanda (hayupo pichani) jijini Dar es Salaam leo.Picha na Mwanakombo Jumaa - MAELEZO.
Na Genofeva Matemu – MAELEZO
Shirikisho la wakurugenzi wa mashtaka Afrika Mashariki limeazimia kuongeza wigo wa ushiriki wa kikosi kazi ndani ya shirikisho hilo ili kuwajibika zaidi na kuweza kupata njia nyingine ya kupanua ushiriki wa waendesha mashtaka binafsi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, rais wa shirikisho hilo Martin Ngoga amesema kuongezeka kwa wigo kutasaidia kuleta ushirikiano wa kutosha na hatimaye kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
“ kwa kipindi hiki uhalifu umekua na changamoto kubwa sana hivyo kufanya kazi kwa pamoja kutasaidia kupanua wigo wa kupata mafunzo ya pamoja kwa wanachama wa shirikisho na kupunguza baadhi ya changamoto hizo”, amesema Ngoga.
Naye makamu mwenyekiti wa shirikisho hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mashtaka kutoka Tanzania Dkt. Eliezer Feleshi amewataka waandishi wa habari kutokujadili na kushadadia kesi zilizoko mahakamani kwani kesi ikiwa mahakamani hairuhusiwi kujadiliwa bali kuiachia mahakama kufanya kazi yake.
Mkutano wa Shirikisho hilo ulioanza jana umemalizika leo ukiwa umehudhuriwa na wakurugenzi wa Mashtaka kutoka nchi tano za Afrika mashariki uliokuwa na lengo la kupitia upya Katiba yao ili kuimarisha umoja wao.