Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyalandu akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa utalii na Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mh. Magessa Mulongo na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini,Mh. Godbless Lema wakitoa msaada wa madawa mbali mbali kwa Hospitali ya St Elizabeth mbele ya Dkt Thomas Kway mganga mkuu wa hospitali hiyo mwenye koti jeupe.na wenye shati jekundu ni Mustapher mkurugenzi wa Bushbuck safaris.
habari/picha na Mahamoud Ahmad wa blog ya jamii Arusha
Serekali na wadau wa utalii wametoa vifaa na madawa mbali mbali vyenye thamani ya Tsh.18 milion kusaidia wahanga wa bomu mkoani Arusha na kuahidi kuanzaisha mfuko wa wahanga wa bomu uwasaidie hata baada ya kupona kwa majeruhi hao na kukusanya kiasi cha 100 milion kuanzisha mfuko huo.
Wakikabidhi kwa pamoja vifaa hivyo naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu alisema kuwa vifaa hivyo ni mwanzo wa kusaidia majeruhi hao na hospitali hiyo ya St. Elizabeth kwani ni hospitali nteule ya halmashauri ya Jiji la Arusha hivyo kusaidia kunahitajika kwa wakati huu ili waweze kwenda na kasi ya wagonjwa wanaofika hospitalini hapo.
Nyalandu akawataka wadau mbali mbali wa sekta ya utalii kufika kwenye hospitali hizo za Mt.Meru,na St.Elizabeth kuona ninamna gain wanaweza kusaidia majeruhi hao waweze kupata matibabu yaliosahihi na kuwa wamejitolea Dakatari bingwa kutoka Hospital ya Agakhan dkt.Aidan Njau kuja kusaidiana na madaktari wa hospital hiyo.
“Tunatarajia kuanzisha Mfuko wa wahanga uitwao Victim Fund utakuwa ukisaidia majeruhi wakati wakiwa hospitali na baada ya hapo tutaendelea kusaidia hadi watakapoweza kuendelea na maisha yao kwa kuanzia mfuko wetu utakuwa na kiasi cha tsh 100 milion”alisema Mustapher mkurugenzi wa Bushbuck Safari ya jijini Arusha
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Magessa Mulongo alisema kuwa serekali imeamua kuwahamisha majeruhi zaidi ya watano kuhamia kwenye hospitali za Lugalo na Muhimbili kwa matibabu zaidi na kuwa pia wamewaleta Madaktari kutoka Kwenye jeshi la wananchi kusaidiana na madaktari kwenye hospitali zetu wakati huu.
Mulongo alisema kuwa Mazishi ya wahanga wa bomu yatafanyika kwenye Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi siku ya Ijumaa na kuwa wanatarajia waziri mkuu Mizengo Pinda ataongoza maelefu ya wakazi wa jiji la Arusha kwenye mazishi hayo kwa niaba ya serekali.
Mulongo alisema huu si wakati wa kuchanganya suala hili na imani za kidini na kisiasa na kuwataka wakazi wa mkoa wa Arusha kutulia na kuacha uchunguzi wa tukio hili uendelee bila ya kutoa manene mbadala.
“Nawasihi sana kutulia na kuwa serekali ipo pamoja nanyi kwenye wakati huu mgumu hivyo tuendelee kuwa pamoja” alisema Mulongo.
Kwa upande wake mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema alisema kuwa anawapa pole majeruhi na wafiwa wawe na moyo wa subra wakati huu wa majonzi na mungu yupo karibu nao huku akiwataka wakazi wa jimbo lake kuwa kitu kimoja kwenye suala hili la wahanga wa mabomu kwa kuondoa tofauti zao za kisiasa.
Makampuni mbali mbali yamekuwa yakijitolea vifaa mbali mbali kwa majeruhi wa bomu kampuni zilizotoa misambali mbali siku ya leo ni pamoja na kituo cha mikutano cha kimataifa (AICC),Viola Safaris,shirika la Msalaba Mwekundu,Ngorongoro Consevetion Athourity na Bushbuck Safari na Hidden Velley Safaris Ltd zote za jijini Arusha.
Vifaa vilivyotolewa na wadau hao ni pamoja na Magodoro,Mablanketi,Madawa ya inana mbali mbali yatakaosaidia wahanga na Hospitali kwa ujumla pia wamekabidhi kwa majeruhi rozali na vitabu vya mafundisho ya imani na vitenge kwa kinamama.
Akikabidhi vifaa hivyo mkuurugenzi wa Viola safaris kwa Mganga mkuu.Mfawizi wa hospitali hiyo Dkt Mlay alisema kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka kwani Hospitali inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo pia chumba cha wagonjwa mahututi(ICU)hivyo akawataka wadau mbali mbali kushiriki kusaidia ujenzi wa wodi hiyo ya wagonjwa mahututi.