Kamati ya maandalizi ya Fainali ya tuzo za Mwanasoka Bora wa mwaka (Wazalendo Footballer of the Year), imeamua kusogezwa mbele kwa fainali hizo ambazo zilikuwa zifanyike Desemba 30 mwaka 2012 jijini Dar es Salaam ambapo sasa zitafanyika Januari 31 mwaka 2013.
Licha ya hatua muhimu kukamilika lakini zipo sababu za msingi ambazo kamati imeona ni busara kuzifuatilia ili kufanya tuzo hizo kufanyika kwa ufanisi.
- Asilimia 90 (90%) ya Wajumbe wa kamati hiyo ni wanachama wa chama cha makocha wa Tanzania (Tafca) ambao wapo kwenye mchakato wa uchaguzi mkuu wa chama chao hivyo kushindwa kukamilisha baadhi ya mambo kwa wakati.
- Pia wapi baadhi ya wageni muhimu ambao walialikwa asilimia (80%) wameonyesha kutokuwepo kwa tarehe hiyo (Demsemba 30, 2012) kwa sababu watakuwa nje ya jiji la Dar es Salaam kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka jambo ambalo kamati imeona pia ni jambo la msingi.
Kwa kuzingatia uzito wa jambo lenyewe kamati imeona ni busara kusogeza mbele kwa siku 30 kwa lengo la kuwapa nafasi wahusika kwa pande zote mbili kuendelea na matayarisho hayo ili kuwa na ufanisi kwenye jambo hili la kitaifa lenye nia ya kusaidia kuinua na kuendeleza vipaji vya soka kwa Watanzania.
Majina yalioingia fainali
Januari Mosi 2013, Kamati ya maandalizi ya tuzo za Wazalendo, inarajia kutangaza majina ya wanasoka ambao wameingia kwenye fainali mwaka 2012. Hatua hii ni baada ya kukamilisha mchujo wa uliokuwa umefanika hapo awali wa kupitia majina zaidi ya 93 yaliyopigiwa kura na mashabiki tangu Agosti-Novemba mwaka huu.
Imetolewa na:-
Ahadi Kakore
- Mratibu.