Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Baraza la Biashara latoa Elimu ya Mashirikiano ya ushindani wa Kibiashara kwa Mikoa ya Kusini,Lindi,Mtwara na Ruvuma

$
0
0
Wadau mbalimbali wa Serikali,Wafanyabiashara na wanahabari toka Mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma wanakutana leo katika warsha ya mashirikiano ya kibiashara kwa mikoa hiyo wanakutana leo ili kujenga na kubadilishana mawazo kwa lengo la kujenga uelewano na Ushirikiano ambao utasaidia kutekeleza Dira ya kibiashara kwa Ufanisi.

Majadiliano hayo ya ushirikiano yatachangia katika kusukuma mbele utekelezaji wa Dira ya Tanzania ya Maendeleo 2025 pamoja na juhudi mbalimbali kuendelea utekelezaji wa Dira hiyo hauendani na shabaha ya kuiwezesha nchi ya kipato cha kati inayojivunia maendeleo makubwa na maisha bora ya wananchi.

Katika warsha hii mada kuu ni kuhamasisha Teknolojia kwa mageuzi ya kiuchumi na kijamii Tanzania itawasilishwa ikienda sambamba na mada ndogondogo ikiwemo Umuhimu wa Ubunifu katika mageuzi ya kiuchumi na kijamii,Mchango wa Tehama,Ubora wa Viwango katika wilaya,usalama wa watu na mali zao ikiwa pamoja na majadiliano ya Vikundi mada ambazo zitatolewa na UDSM,COSTECH,TCRA,TBS na Polisi Makao Makuu
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara,Kanali Joseph Simbakalia akifungua Warsha ya Majadiliano ya Ushirikiano wa Kibiashara kwa Manufaa ya Umma Kikanda kwa Wawakilishi toka Mikoa ya Lindi,Ruvuma na Wenyeji Mtwara,Kulia ni Samson Chemponda,Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara na kushoto ni Saidi Masudi Nahunda,Mwenyekiti wa TCCIA-Mtwara.
Wadau mbalimbali wanaohudhuria kikao cha mashirikiano ya kibiashara kutoka mikoa ya Lindi Mtwara na Ruvuma kinachoendelea katika Ukumbi wa Makonde Beach Resort-Mtwara.  Na Abdulaziz Video-Mtwara

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>