Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115280

Kigwangalla ajibu tuhuma za ufisadi kupitia misamaha ya kodi

$
0
0
Dkt Hamisi Kigwangwalla


Bungeni, Dodoma, Mei 1, 2013.
 Nawasalimu kwa heshima na taadhima.
Napenda kutumia fursa hii kutoa taarifa kwa wanahabari na umma kwa ujumla kufuatia habari iliyotoka leo mapema asubuhi kwenye gazeti la Sauti ya watu Tanzania Daima, toleo Na.3071 na kuzua mjadala mkubwa na mzito kwenye jamii pamoja na kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na hadhi, heshima na uadilifu wangu kwenye jamii nikiwa kama kiongozi wa umma. Niwape pole wale wote walioguswa na kushughulishwa na jambo hili, haswa familia yangu, ndugu, marafiki na wananchi wa Nzega; ambao siku zote wanaamini sana katika uadilifu wangu na namna ninavyosimamia misingi ya haki, sheria na uzalendo.

Nimesikitishwa sana na habari  hii hususan kwa kuwa ilichapishwa bila kunipa fursa ya kueleza kwa mapana uhusika wangu. Niwapongeze gazeti la Nipashe kwa kupuuza uzushi huu mara baada ya kunipigia na kueleza upande wangu wa hadithi.

Kumekuwa na wimbi kubwa la baadhi ya watu kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuandika habari za uongo kwa maslahi maovu ya kuwachafua wanasiasa na watu wengine. Watanzania sote tubadilike na tukatae tabia za kutumika vibaya namna hii, maana ni hatari kwa ustawi wa weledi, na kwa umoja na mshkamano wa kitaifa. Ukishaandika jambo ambalo litamchafua mwenziyo, hata kama utamsafisha kiasi gani ni wazi hautokuwa na uhakika kuwa utawafikia wale wale waliosoma zile za jana za kumchafua – hivyo ni jambo la kawaida kabisa kuanza kwanza kwa kuwa na uhakika kabisa na habari kabla ya kuiandika. 

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115280

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>