Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akiongea katika hafla fupi ya kufunga mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika hilo kuhusu Ujasiriliamali katika wilaya ya Ilala.Mkutano huo ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya vijana na Maafisa wa Serikali.
Meneja Miradi wa Shirika la Plan International Wilaya ya Ilala Daniel Kalimbya akiongea katika hafla fupi ya kufunga mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika hilo kuhusu Ujasiriliamali katika wilaya ya Ilala.Mkutano huo ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya vijana na Maafisa wa Serikali.
Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa tathmini ya miradi inayoendeshwa na Shirika la Plan International kuhusu Ujasiriliamali wakimsikiliza mgeni rasmi katika hafla ya kufunga mafunzo hayo wilayani ya Ilala.Mkutano huo ulishirikisha wadau kutoka Asasi zisizo za kiserikali, Vikundi vya vijana na Maafisa wa Serikali.(Picha na Frank Geofray)
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw.Raymond Mushi amevitaka vikundi vya Vijana, Asasi zisizo za Kiserikali na watumishi wa umma waliopata mafunzo ya ujasiriliamali yanayotolewa na Shirika la kimataifa la Plan kuyatumia vizuri katika kuwaletea maendeleo na kuondokana na umaskini.
Bw.Mushi aliyasema hayo wakati alipokuwa akifunga mkutano wa kufanya tathmini ya miradi ya ujasiriliamali iliyokuwa ikiendeshwa na shirika hilo kwa makundi mbalimbali katika kata zote za wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam.
Alisema ujasiriliamali ni njia mojawapo ya kuondokana na umaskini na kujikwamua kiuchumi hivyo kutolewa kwa mafunzo hayo kutawasaidia wananchi kutambua fursa zilizopo na kuzitumia vyema.
Aidha aliwaasa washiriki wa mkutano kuwekeza katika elimu kwa watoto ili kujenga taifa lenye uelewa na maarifa hapo baadae kwa kuwa watoto wanapaswa kupewa haki yao ya kupata elimu bora.
“Pamoja na kwamba mtawekeza katika kufanya biashara lakini lazima mhakikishe na suala la elimu kwa watoto wenu mnalitilia mkazo ili kuweza kuwajengea maisha bora hapo badaye”Alisema Bw.Mushi.