Globu ya Jamii imepokea kwa mshituko mkubwa na simanzi taarifa kuwa Bi Kidude katutoka. Tunatoa salaam za rambirambi kwa watu wote wa Zanzibar pamoja na wa Bara waliomuenzi msanii huyu ambaye pamoja na umri wake mkubwa aliendelea kutuliwaza kwa usanii wake jukwaani pamoja na matani na ucheshi usio kikomo nje ya jukwaa. Kuna wachache wa aina yake Wallahi..
Akiwa ni mmoja wa wasanii nguli Bara na Visiwani, Bi Kidude alikuwa karibu sana na Globu ya Jamii kiasi ya kwamba pamoja na umri wake mkubwa, mara kadhaa alikuwa anatutia moyo wa kuendeleza libeneke kwa namna ambayo haitoweza kusahaulika.
Alikuwa mtu wa karibu sana na Ankal, ambaye hata katika hali yake ya kudhoofu kutokana na umri na maradhi hakukosa kumtambua na kumtania. Ankal ni mmoja wa wanaLibeneke wachache ambao Bi Kidude aliwakubalia kupozi kupigwa picha nao.

Ni kweli kwamba kila mtu ataonja mauti, lakini si uwongo kwamba kuondokewa na kipenzi chetu Bi Kidude ni pigo kubwa kwa Globu ya Jamii kama ilivyo kwa jamii yote ya tasnia ya sanaa katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MOLA AIWEKA MAHALA PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU BI KIDUDE
AMEN