Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam, hatua ya sita bora imeanza jana Aprili 15 katika viwanja vitatu na matokeo yalikuwa kama ifuatavyo:
Uwanja wa Makurumla- Red Coast iliichapa Abajalo FC 1-0. Bao hilo lilifungwa na Rashid Juma. Uwanja wa Airwing-Shariff Star iliifunga Boom FC 1-0. Bao hilo lililifungwa na Mandewa Mrutu ‘Niyonzima’.
Uwanja wa Kinesi-Friends Rangers vs Day Break hazikufungana.
Ligi hiyo itaendelea Alhamisi, Aprili 18, ambapo Boom FC itacheza na Day Break, kwenye uwanja wa Airwing, wakati Friends Rangers wao watachuana na Red Coast kwenye uwanja wa Kinesi, huku Abajalo wakichuana na Sharif Stars kwenye uwanja wa Msasani.
Imetolewa na Mohamed Mharizo
Ofisa Habari Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).