Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

BodaBoda wapo juu ya sheria nchini??

$
0
0
Waendesha pikipiki zinazopakia abiria maarufu kama Boda Boda wako juu ya sheria na hakuna mtu anayeweza kutia fyoko, Globu ya Jamii inaweza kuthibitisha. Waendesha Boda Boda jijini Dar es salaam na hata mikoani wameanzisha himaya yao inayoonesha hata vyombo vya dola havina ubavu kuidhibiti, hata kama ni kuchukua sheria mikononi watakavyo na kuvunja sheria za usalama barabarani. 

Wananchi wengi tuliowahoji wametahadharisha kwamba endapo vyombo vya dola vitaruhusu hali hii iendelee, usalama na amani nchini vinaweza kuwa rehani kimoja. Wamehoji kwa nini hawa waendesha BodaBoda wamekuwa wajeuri na wababe dhidi ya wananchi tena mbele ya dola? "Bwana mwandishi ka ma unabisha hebu mgonge kwa gari Bodaboda mmoja uone jioni wenzie toka kila kona watakavyokutanika na kukushambulia na kukudhuru", anasema Mwananchi mmoja, akiendelea kushangaa pale Bodaboda wanapoachiwa kuvuka wakati taa za barabarani kuwa nyekundu. 

Globu ya Jamii jana Jumapili ilishuhudia Bodaboda wakitawala barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam wakati wakisindikiza gari linalosadikiwa kuwa na mwili wa mwenzao aliyefariki dunia, akipelekwa maeneo ya Ukonga kwa maziko. Kwenye makutano ya njia inayoelekea Uwanja wa Ndege wa kimataifa ya Julius Nyerere, ambapo pana taa za barabarani, umati huo wa Bodaboda ulifanya ubabe kupita wakati taa zilikuwa zinawaka nyekundu na hata askari trafiki aliyekuwepo pale alidharauliwa na badala yake mmoja wao ndio akawa anaongoza magari. 

Pia Daladala moja lililojaa abiria  lililazimishwa kibabe na kwa matusi kupaki pembeni ili msafara wa Bodaboda upite, na dereva alipotaka kungoja taa ziwake za kijani ili aendelee akazingirwa na Bodaboda kibao hadi akasalimu amri. Hali hii inazidisha maswali kwani hawa watu ni kina nani wafanye watakacho bila kujali sheria halali za nchi? 

Wananchi wametoa wito kwa wahusika kutathmini hali hii ambayo wameitaja kama bomu linalofukuta, na kisha kuchukua hatua haraka sana kabla hali haijawa mbaya zaidi ya ilivyo sasa. Vile vile wameshauri kuwepo namna ya kuwaelimisha Bodaboda namna bora ya kuendesha shughuli zao kwani kwa mfano mdogo tu wengi hawana utaalanmu wa kuendesha pikipiki, hali inayopelelea kukuta majeruhi wengi katika hospitali zote hivis sasa ni Bodaboda. 

"Hawa wanahitaji elimu ya namna ya kuendesha pikipiki ama sivyo tutapoteza vijana wetu kila siku" kasema mwananchi mwingine, akitolea mfano wodi ya Sewa Haji ya Taasisi ya Mifupa (MOI) iliyoko Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambapo kwa uchache tu waendesha Bodaboda 15 hulazwa pale kwa majeraha kwa siku.
Bodaboda wakiteka barabara ya Nyerere jijini Dar es salaam
Mpita njia amepigwa butwaa kuona Bodaboda wanalazimisha Daladala lipaki pembeni ili wao wapite
Wengi ni vijana wadogo wa umri kati ya miaka 15 na 30.
Daladala likilazimishwa kupaki pembeni
Abiria wanashangaa kuona Bodaboda wakifanya watakalo
Gari walilokuwa wanalisindikiza likipita
Daladala limezingirwa na Bodaboda
Mmoja wa waendesha Bodaboda akielekeza pikipiki zipite huku daladala likiwa limesalimu amri na kupaki pembeni

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles