Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

KATIBU MKUU KIONGOZI BALOZI OMBENI SEFUE ATEMBELEA MRADI WA JENGO JIPYA LA OFISI YA MKUU WA MKOA DODOMA

$
0
0

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa tatu kushoto) akitoa maelekezo alipotembelea mradi wa ujenzi jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.

Mafundi wa kampuni ya China Railway Jiachang Engeneering Ltd (CRJE Co. Ltd) inayojenga Jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiendelea na kazi kama walivyokutwa na Katibu Mkuu Kiongozi (hayupo pichani) mwishoni mwa wiki alipotembelea mradi huo.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watumishi wa serikali kutambua kuwa wanawajibu mkubwa wa kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma hapa nchini kupitia utendaji uliotukuka.
Balozi Sefue alieleza hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ambapo alisisitiza kuwa watendaji na viongozi wote wa umma kuanzia ngazi za chini za uongozi na utumishi wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo na kuondoa taswira mbaya inayouandama utumishi wa umma.
Katika hatua nyingine baada ya katibu Mkuu Balozi Sefue kuona tatizo la ukosefu wa ofisi kwa watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma na kutembelea mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma unaokwenda taratibu kutokana na upatikanaji wa fedha, balozi Sefue amesema serikali inawajibu wa kuhakikisha mradi huo unakamilika haraka iwezekanavyo.
Vilevile ameahidi katika mwaka wa fedha ujao 2013/14 serikali inaweza kutoa mara mbili ya fedha zilizoombwa na sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya uendelezaji wa ujenzi wa mradi huo wa ofisi ambapo jumla ya shilingi bilioni tatu ziliombwa kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika bajeti ya mwaka 2013/14.
Kwa upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge alibainisha kuwa pamoja na tatizo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutokuwa na jrngo lake la ofisi, matatizo mengine yanayoikabili sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ni pamoja na Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha kidogo za kuendeshea ofisi wakati gharama za uendeshaji zinapanda.
Aidha uchache wa watumishi hasa kwenye kada za afya ni tatizo linguine lenye kuhitaji utatuzi na kumuomba katibu mkuu kiongozi kutoa vibali kwa maombi yote ya kuajiri yatayomfikia mezani kwake na kuiomba serikali itenge bajeti ya kuajiori watumishi wa kada zenye upungufu ili sekretarieti za Mikoa ziweze kuajiri na kuziba nafasi wazi.
Akiwakilisha watumishi wengine, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dr. Lucy Mkandawile alisema kuwa matatizo mengine yanayogusa watumishi moja kwa moja ni pamoja na uchelewaji kupanda vyeo, malimbikizo ya Mishahara baada ya kupanda vyeo, malipo ya nauli za likizo na matibabu, fedha kwa ajili ya sare za kazi, ufadhili wa masomo kwa watumishi kwa ajili ya kujiendeleza na mishahara midogo.
Akijibu hoja hizo katibu Mkuu alieleza kuwa serikali inazifahamu baadhi ya changamoto zilizoelezwa na inazichukua zote pamoja na zile mpya zinazoendelea kuibuliwa na kuahidi kuwa serikali itaongeza jitihada katika kuzishughulikia lengo likiwa kuzidi kuboresha mazingira ya utumishi wa umma na hali za maisha za watumishi.





Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>