Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

MATUNDA YA BIMA INAYOFUATA SHERIA ZA KI-ISLAM

$
0
0

Moja ktk  tofauti kubwa iliyopo kati ya bima inayofuta sheria za ki-Islam na ile isiyofuata sheria ya ki-Islam ni kitendo cha wateja kugawiwa faida inayopatikana ktk biashara hiyo.

Takaful Insurance of Africa Limited (TIA) ni shirika la bima la kwanza nchini Kenya linalofuata sheria za ki-Islam ambalo limetangaza kugawana faida na wateja wake. Ktk kongamano lililohudhuriwa na mashirika yasiyopungua 500 ambayo ni wateja, brokers na mawakala, TIA ilitangaza kugawana asilimia 60 ya faida na wateja wake 4000 ambao hawakudai fidia yoyote ktk kipindi cha mwaka mzima. 

Alinukuliwa akisema mwenyekiti wa shirika hilo ndugu Abdurahman Sheikh ‘ninayo furaha na heshima kubwa kutangaza kwamba TIA imepata ziada (Surplus) yake ya kwanza ambayo ni sawa na Sh 15.6 million za Kenya na ambazo watagawana na wateja wake’, ktk tukio ambalo ni lakwanza kwa shirika la bima kufanya hivyo Kenya na Africa Mashariki kwa ujumla.

Akizungumza ktk kongamano hilo Mkurugenzi Mkuu Ndugu Hassan Bashir alisema ‘shirika limekua sana ukilinganisha na lilivyoanzishwa miaka miwili iliyopita, na limeweza kufanya kwa kipindi hicho, kile ambacho mashirika mangine yamekifanya kwa muda usiopungua miaka kumi’. Kwa maelezo zaidi kuhusu bima inayofuta sheria za ki-Islam wasiliana na http://ijuebankyakiislam.blogspot.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>