Mheshimiwa Angellah Kairuki (MB), Naibu Waziri wa Katiba na Sheria akiwa na mwenyeji wake Mhe. Sayid Ashraful Islam, Waziri wa Serikali za Mitaa, Maendeleo Vijijini na Ushirika, (Wizara inayoshughulika na Usajili wa Vizazi naVifo) wakati wa ziara yake nchini Bangladesh kujifunza namna ambavyo nchi hiyo imeweza kufikia asilimia zaidi ya 95 ya usajili wa Vizazi naVifo.
MheshimiwaAngellah Kairuki, Naibu akijibu maswaliyawaandishi wa habari wa Bangladesh
Mheshimi wa Angellah Kairuki akifafanua jambo kwa Mhe. Hassanul Haq Inu, Waziri wa Habari wa Bangladesh wakati walipokuwa wakisubiri kukutana na waandishi wa habari wa Bangladesh na kueleza madhumuni ya ujumbe wa Tanzania kwenda nchini Bangladesh kujifunza namna ya kuboresha mfumo wa usajili wa vizazi na vifo hadi kufikia asilimia mia moja (100%).
Mhe. Angellah Kairuki akielezwa jambo na Bw. Nazrul Islam, MtendajiMkuu wa Dhaka South City Corporation
Mhe. Angellah Kairuki akiwa na Sir. Fazle Abed, Mwanzilishi na Mwenyekiti wa taasisi ya BRAC alipotembeleaMakaoMakuuya BRAC.
Mhe. Angellah Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wake wa wataalam kutoka Taasisi za RITA, NIDA, TRA, Serikali za Mitaa, e-Government, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Ofisi ya Takwimu,,Ofisi ya Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na wenyeji wake.