Mkuu wa Wilaya Kilwa,Abdala Ulega akitoa maagizo wakati alipokuwa akizungumza na wazazi,walezi na wadau wa elimu katika shule ya sekondari mibuyuni wilayani humo jana
Baadhi ya Wazazi,Walezi na Wadau wa Elimu waliofika shuleni hapo.
serikali ya wilaya ya kilwa imewataka wazazi na walezi wanaowakataza watoto wao kwenda shule wachukuliwe hatua za sheria ili kukomesha vitendo hivyo.
Agizo hilo limetolewa na mkuu wa wilaya Kilwa Abdala Ulega wakati alipokuwa anazungumza na wazazi walezi na wadau wa elimu wa shule ya sekondari mibuyuni wilayani humo jana.
Ulega alisema kufanya hivyo sio tu kwamba ni kuwa nyanyasa bali pia ni kuwanyima hakiyao ya msingi na urithi wa maisha yao ya baadaye watoto ambao ndiyo tegemeo la taifa.
Watendaji wa tarafa, kata, kijiji wametakiwa kutekeleza agizo hilo kwa kuwachukulia hatua wazazi na walezi aina hiyo.
Alisema kuwa kuwakataza watoto kwenda shule mbali na kuwanyima haki zao vilivile kunakwamisha juhudi za serikali za kukuza elimu.
Ulega alitoa agizo hilo baada ya kupata taarifa kuwa zaidi ya watoto 200 wa shule ya sekondari Mibuyuni hawafiki shuleni kutokana na utoro wa rejareja na kusababisha shule hiyo kuwa na mahudhurio madogo kila siku.
Aidha shule ya sekondari mibuyuni ambayo iko katika wilaya Kilwa Mkoani Lindi ni kati ya shule 10 zilizofanya vibaya katika matokeo ya kitado cha nne mwaka huu.