Tarehe 10/04/2013 taasisi ya wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro (WAVUMO) ambayo ni shirika lisilo la kiserikali na lisilotengeneza faida, waliandaa harambee kwa maendeleo na kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Ukimwi kwamba Ukimwi sio tatizo la Afya tu bali linahusu maendeleo ya Jamii kwa ujumla. Harambee hiyo yenye nia ya kujikwamua badala ya kutegemea wafadhili kutoka nje iliweza kufanikiwa kupitia watu na jamii mbalimbali ya Morogoro kutokana na mioyo yao mizuri na kwa michango yao. Mgeni rasmi alikuwa Mh. Mkuu wa Mkoa aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI.
Shirika ili la Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Morogoro (WAVUMO) pia liliandaa chakula cha usiku katika kufanikisha harambee hiyo. kauli mbiu ilikuwa, "MLO WA JIONI KWA KUOKOA MAISHA / A DINNER A LIFE SAVED". Harambee hii ilifanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha 11,000,000/=, mradi wa soda kreti 15, friji kubwa, meza mbili na viti nane kutoka pepsi, vilevile ilifanikiwa kupata plot za Ardhi kwa ajili ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji cha mpunga ambacho kitakuwa kinaendelea kutunisha mfuko wa WAVUMO.
Shirika la WAVUMO linawanachama zaidi ya 500 na linahudumia wagonjwa wa Ukimwi zaidi ya 3000 kwa manispaa ya Morogoro. Shirika lina miaka 12, kwa sasa linaongozwa na Mwenyekiti Bw. Ally Ramadhani.
Kwa maelezo zaidi kuhusu harambee hii na taasi ya WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI MOROGORO (WAVUMO), Wasiliana nao kupitia +255 714 255 688, au +255 767 245 688.
Zoezi la Harambee likiwa limefunguliwa rasmi na Mgeni rasmi, kutoka kulia ni Mratibu wa Harambee, Mourine-Hawa Msangi na Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Manispaa Mheshimiwa SAID AMANZI.
Mr. Signfrid Kayombo na Mr Mujungu Wajama ambao ni Wawakilishi kutoka TUNAJALI wakiotoa mchango wao.
Mr. Juma Ayoub Bitagera kutoka NIC akitoa mchango wao.