Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Zenno Ngowi akiongea wakati wa uzinduzi wa maonyesho ya 3 ya Tanzania Homes Expo yanayotarajiwa kufanyika Juni 2013. Kushoto ni mratibu wa maonyesho hayo Happy Geddi na kushoto ni Meneja Masoko Mesha Gobba.
Maonyesho ya tatu ya Tanzania Homes Expo yanatarajiwa kufanyika Mlimani City Juni 2013 na kushirikisha makampuni pamoja na taasisi mbalimbali za sekta ya nyumba Tanzania na Kenya. Mara ya mwisho maonyesho hayo yalifanyika Desemba 7 hadi 9 2012.
Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kufanyika kwa maonyesho hayo, Mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo, ndugu Zenno Ngowi alisema, “Katika maonyesho hayo, watoa huduma wa sekta ya nyumba kama makampuni ya nyumba, wachora ramani, bima, makampuni ya ulinzi, mikopo, bima, wakandarasi na wengine wengi watapata fursa ya kuelezea huduma wanazozitoa.
Tanzania Homes Expo, itazialika taasisi zinazohusika na ujenzi kushiriki kwenye maonyesho yajayo ili kutoa elimu kwa uma. Kuna msemo maarufu usemao ‘’kutokujua sheria haihalalishi kutenda kosa’’. Kwetu sisi tunaamini Tanzania Homes Expo inatoa fursa nzuri kwa jamii yetu kupata taarifa na kujua masuluhisho mbalimbali ya ujenzi”.
Kuhusu ushiriki wa makampuni kutoka Kenya, mkurugenzi wa Tanzania Homes Expo Bwana Zenno Ngowi alisema “Tunaamini kupanuka kwa wigo wa washiriki toka kwenye Nchi ya jirani kutatoa fursa ya Wananchi kupata masuluhisho mbalimbali ya ujenzi. Nishati mbadala, ni eneo jingine ambalo tunategemea kupata washiriki wengi wapya ambao watakuja kuonyesha masuluhisho mbalimbali ya nishati mbadala”.
Kwa taarifa zaidi au kushiriki tembelea tovuti;
www.eaggroup.co.tz au tuma barua pepe info@tanzaniahomesexpo.org