Mkufunzi kutoka Uingereza, Bw. David Wiggins, akiwaaga Maafisa Mawasiliano Serikalini (hawapo pichani) baada ya kumaliza mafunzo katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) .
Hivi karibuni Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uingereza nchini imewapatia mafunzo ya kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii katika kuimarisha mawasiliano. Mafunzo hayo yameendeshwa na Taasisi ya Thomson Foundation na kugharamiwa na Serikali ya Uingereza. Pichani Mkufunzi wa Mafunzo David Wiggins (katikati) akifurahia zawadi ya shati la kitenge baada ya kukabidhiwa na Afisa Mawasiliano kutoka Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi Judith Mhina (kushoto ) kwaniaba ya wenzake, (kulia) ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari Assah Mwambene.
Maafisa Mawasiliano Serikalini wakiwa katika picha ya pamoja. baada ya kumaliza mafunzo ya jinsi ya kutumia mitandao ya kijamii kama facebook,twitter, flickr na blogs.