Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo (MB) akibonyeza kitufe kwenye kompyuta mpakato (laptop) kuashiria uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo (MB) akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii,Mh. Lazaro Nyarandu (MB) akizungumza wakati wa tafrija ya uzinduzi rasmi wavuti ya www.shuledirect.co.tz. Mtandao unaowawezesha wanafunzi wa elimu ya Sekondari na jamii ya Tanzania kwa ujumla kujifunza kupitia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
Mratibu Mwanzilishi wa Kampeni ya ShuleDirect, Faraja Kotta Nyalandu akifafanua jambo wakati wa tafrija hiyo iliyofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.Faraja alisema kuwa ili malengo ya nchi yetu hasa kwenye elimu bora yafikiwe, ni muhimu kila mtu katika Nyanja na maisha yake atimize wajibu wake, na hata wakati mwingine achukue wajibu ambao si wake na aliendelea kusema kuwa inatupasa wote tuchanganye uzoefu, maarifa, ujuzi, miundombinu, rasilimali za wengi ili kufikia malengo ya nchi yetu.
Mratibu Mwanzilishi wa Kampeni ya ShuleDirect, Faraja Kotta Nyalandu (pili kushoto) akiwa na Jacqueline Ntuyebaliwe,Ally Remtullah na Mdau.
Naibu Waziri wa Elimu na Ufundi Mhe. Phillip Mulugo akifurahi jambo na baadi ya wanafunzi wa shule za sekondari waliokuwepo kwenye uzinduzi huo wakati akiwaonyesha kitu kutoka kwenye kompyuta.