Picha na Habari-Mdau Abdulaziz Video,Lindi
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya umeandaa huduma za madaktari bingwa kutoka hospitali ya Rufaa MUHIMBILI watakaotoa huduma katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi (SOKOINE) kuanzia tarehe 8.4.2013 hadi tarehe 13.4.2013.
Uzinduzi wa huduma hiZi utafanywa rasmi siku ya jumatatu(KESHO) tarehe 8.4.2013,Mgeni rasmi ni mkuu wa mkoa wa Lindi pia uzinduzi huo utahudhuriwa na Mkurugenzi mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya,Ndg Emmanuel Humba.
Akitoa taarifa hiyo kwa Waandishi wa Habari,Meneja wa ofisi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Lindi,Bi Fortunata Kullaya alieleza kuwa hatua hiyo imekuja ili kusaidia huduma kwa wateja wa Mfuko huo na wagonjwa wengine ambapo wagonjwa wasio wateja wa Mfuko watatumia taratibu za kawaida zilizopo katika kupata matibabu.
Hivi karibuni Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Kwa kushirikia na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo(WAMA)imetoa mafunzo kwa vikundi mbalimbali vya wajasiliamali katika wilaya za Lindi na Kilwa ili wajiunge na mfuko wa Afya ya Jamii(CHF) NA Kutoa msaada wa Mashuka kwa Hospital za Wilaya ya Ruangwa na Kilwa
Meneja wa Ofisi ya Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya-Lindi,Bi Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya ujio wa Madaktari Bingwa wanaoletwa na Mfuko huo na kuhudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF kesho katika hospital ya Sokoine Lindi
Viongozi wa mfuko wa NHIF pamoja na WAMA wakiwa wameketi pamoja chini na waliohudhuria katika Elimu elekezi kwa vikundi vya wajasiriamali kujiunga na CHF Iliyofanyika katika kijiji cha Namangale-Lindi Vijijini