Hapa ndipo alipopigwa risasi na kuuwawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Makamu wa pili wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mzee Abeid Amani Karume wakati akicheza bao na marafiki zake katika makao makuu ya CCM Kisiwandui, Unguja. Matundu yanayookekana kwenye ukuta ni ya risasi zilizomiminwa na muuwaji ambaye naye aliuwawa na walinzi wa Mzee Karume, mnamo Aprili 7, 1972. Chini wanafunzi wakiiangalia sehemu hiyo ambayo haijaguswa wala kuondolewa kitu na imewekwa uzio kuihifadhi kama kumbukumbu
Sanamu ya Mzee Abeid Amani Karume ikiwa mbele ya Ofisi Kuu ya CCM Zanzibar, Kisiwandui,