Mzee Hamza Kasongo (kati) akibadilishana mawazo na Balozi Christopher Liundi (shoto) na mwandishi wa habari mkongwe Mzee Fred Jim Mdoe katika hafla ya siku za nyuma. Mzee Kasongo usiku huu ameibuka kidedea kwa kutwaa TUZO YA MAISHA YA MAFANIKIO KATIKA TASNIA YA HABARI kwenye hafla inayoendelea hivi sasa katika ukumbi wa Diamond Jubilee hall jijin Dar es salaam, mgeni rasmi akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Shariff Hamad kwa niaba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Mohamed Ali Shein.
Mzee Hamza Kasongo mwenye umri wa miaka 74, ni mtangazaji mkongwe wa radio na TV, alikuwapo kama mtangazaji wakati wimbo wa Taifa ukipigwa kwa mara ya kwanza kwa kutajwa Tanzania badala ya Mungu Ibariki Tanganyika siku ya uhuru mwaka Desemba 9, 1961, ambapo aliwasiliana moja kwa moja na Alex Nyirenda wakati akipandisha mwenge mlima Kilimanjaro.
Mzee Hamza Kasongo alikuwa miongoni mwa vijana saba waliochaguliwa kupata mafunzo ya utangazaji wa Sauti ya Dar es salaam, kabla ya RTD miaka ya 60.
Baada ya Uhuru, akiwa na hayati Salim Seif Mkamba na David Wakati (RiP) January 1962 walipata nafasi ya kwenda kupata mafunzo ya utangazaji jijini London, Uingereza, katika Shirika la Habari la BBC na kutangaza. Mwaka 1965 alirejea na kuwa mkuu wa habari na matukio RTD. Baada ya miaka kupita akajiunga na Africa Media Group na kuwa Mkurugenzi wa Habari wa Channel Ten ambapo hadi leo anaendesha kipindi cha Wasaa wa Hamza Kasongo, akimuachia Jenerali Ulimwengu kundesha kipindi kilichochukua nafasi ya Hamza kasongo Hour.

Mshindi wa jumla ya uandishi wa habari umeenda kwa mpiganaji Lucas Liganga wa The Citizen. Tuzo hizi za kila mwaka zimeandaliwa na Baraza la Habari Tanzania.