Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman ............................................................. Taarifa kutoka Tunduma mkoani Mbeya zinadai kuwa hali si shwari katika eneo hilo kutokana na kuzuka kwa vurugu kubwa zinazodaiwa kusababishwa na masuala ya kiimani ya nani achinje kati ya mkristo na Muislam . Habari zinasema vurugu hizo zimeanza majira ya saa nne asubuhi kwa makundi ya vijana kuandamana mitaani na kuvutana kuhusu uamuzi wa viongozi wa dini ya kikristo Tunduma kuandika barua kwa mkuu wa wilaya kutaka kuruhusiwa kuchinja wakati wa Pasaka. Insemekana kuwa kabla ya Ijumaa kuu viongozi hao wa dini ya Kikristo walikutana na mkuu wa wilaya Mhe. Momba Abuud Saidea ambae aliwataka kuwasilisha barua rasmi ya kufanya hivyo . Hata hivyo inaelezwa kuwa vurugu hizo za leo hazina mahusiamo ya moja kwa moja na masuala ya dini kwani wanaoshiriki katika vurugu hizo ni vijana wapiga debe ambao baadhi yao wamechanganyika na vibaka kwa lengo la kuchafua hali ya hewa, kwani suala la uchinjaji ambalo lilifanyika siku ya Pasaka halikuwa na mvutano wowote baada ya wakristo kuchinja katika bucha zao na waislamu hao kuchinja katika mabucha yao na kila mmoja kufanya biashara kwa kupata wateja wake kama kawaida . Ila katika hali ya kushangaza ni baada ya leo kuibuka kundi hilo la vijana wanaofanya kazi katika stendi na vijiwe mbali mbali kuanzisha vurugu kiasi cha polisi kuingilia kati kwa kutumia mabomu ya machozi na kuwatawanya wananchi waliokuwa wamekusanyika maeneo mbali mbali . Kutokana na vurugu hizo mpaka wa Tunduma ambao unaingia nchi za kusini wa Tanzania ulifungwa pamoja na magari yaliyokuwa yakitoka Sumbawanga pia kuzuiwa kuendelea na safari hadi hali hiyo ilipotulia mida hii saa 8 mchana baada ya kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman kufika eneo hilo. |
↧
VURUGU ZAIBUKA TUNDUMA LEO
↧