Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

SHUKRANI

$
0
0
Marehemu Peter Cuthbert Samatta

Familia ya Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas A. Samatta wa Oyster Bay, Dar Es Salaam na Bibi Trinita Samatta wa Singida tunatoa shukrani zetu kwa wale wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kutufariji katika msiba wa mpendwa wetu Peter Cuthbert Samatta aliyefariki katika Hospital Kuu ya Taifa Muhimbili tarehe 11 Frebruari, 2013 na kuzikwa kwenye Makaburi ya Kinondoni hapa Dar Es Salaam tarehe 14 February 2013.

Shukrani za pekee ziwafikie wafutao. Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete; Mheshimiwa Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman; Waheshimiwa Majaji wa Mahakama ya Rufaa na Mahakama Kuu; Waheshimiwa Majaji wastaafu; Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe na Mama Membe; Mheshimiwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta na Mama Sitta.

Menejimenti na Watumishi wa Shirika la Taifa la Bima; Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe; Profesa Mkude; Makamu Mkuu wa Chuo Cha Mzumbe Profesa Joseph Kuzilwa na Makamu wake Maprofesa F. kamuzora na J. S. Itika.

Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Sigara Tanzania (TCC) Bwana Majid Abdo; Menejimenti na Watumishi wa MDH (Management Development for Health); Menejimenti na Watumishi wa ESOS. Madaktari na Manesi wa Mwaisela Wodi Number 08 Hospital Kuu ya Taifa ya Muhimbili na wale Hospital ya Misheni ya Makiungu, Singida.

Wanachama wa Green Women Group na waume zao; Majirani wa Mtaa wa Bongoyo Oyster Bay na Mitaa inayopakana na Mtaa huo; Majirani wa Oyster Bay Neighborhood Association (CONA); Bibi Elizabeth Mwella; Majirani wa Familia ya Marehemu Mjini Singida; Walimu wenzie wa Mjane wa Marehemu Trinita; Viongozi wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Upanga, Dar Es Salaam; Kwaya ya Kanisa hilo; Wanajumuia wa Jumuia ya Mtakatifu Agostino wa Hippo; Ndugu, Jamaa na Marafiki.

Ibada ya Shukrani itafanyika katika Kanisa la Mtakatifu Albano siku ya Jumamosi tarehe 6 April, 2013, kuanzia saa mbili asubuhi. Karibuni.

“MPENDWA WETU PETER MIKONONI MWA MWENYEZI MUNGU PUMZIKA, MIOYONI MWETU ISHI DAIMA”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>