Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

huduma mpya ya Airtel Yatosha yapokelewa kwa kishindo ndani ya morogoro.

$
0
0

Pichani kushoto ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha pamoja na Muda wa maongezi kwa mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema,kulia ni Meneja Mauzo wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Morogoro,Aluta Kweka.
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop, kutoka kundi la Tip Top Conection ajulikanae kwa jina la Madee a.k.a Rais wa Manzese akiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na wimbo wake wa “NANI KAMWAGA POMBE YANGU”,wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.
Sehemu ya Umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel Yatosha ndani ya mkoa wa Morogoro.
Wakazi wa morogoro walijitokeza kwa wingi jukwaani kujiunga na huduma ya Airtel yatosha kwa Kupiga *149*99#.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya,Ney wa Mitego akitumbuiza mbele ya umati wa wakazi wa mji wa Morogoro waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha ndani ya mji huo.Huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.

Pichani kulia ni Meneja Mahusiano wa kampuni ya simu za mikononi ya Airtel-Tanzania,Jackson Mmbando akimkabidhi fulana ya Airtel Yatosha mmoja wa watumiaji wa huduma hiyo mara baada ya kueilezea vyema huduma hiyo mbele ya  wakazi wa mji  huo na vitongoji vyke,Katikati ni Msanii Nguli wa muziki wa kizazi kipya wa hip hop Fid Q akishuhudia tukio hilo.
Msanii Mkongwe wa muziki wa kizazi kipya Juma Nature akiwa sambamba na baadhi ya wasanii wenzake wanaounda kundi la Wanaume TMK-Halisi wakiwarusha vilivyo wakazi wa mji wa Morogoro na Vitongoji vyake wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya  Airtel Yatosha ndani ya mji wa Morogoro jana jioni kwenye viwanja vya shule ya msingi Sabasaba.

Sehemu ya umati wa wakazi wa morogoro uliofurika kwenye uwanja wa shule ya msingi Sabasaba wakati wa uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel  Yatosha wakishangilia,huduma hiyo itatambulishwa tena  hivi karibuni  kwa wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 115264

Trending Articles